24 Desemba 2018 - 17:35
Rais wa Uturuki: Netanyahu ni sauti ya madhalimu duniani

Rais wa serikali ya Uturuki amemshambulia vibaya waziri mkuu wa Utawala haramu wa Israel na kusistiza kuwa Netabyahu ndio sauti ya madhalimu duniani

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: hayo yamesemwa na Recep Tayyip Erdogan, ambaye ni Rais wa serikali ya Uturuki na kusema kuwa waziri mkuu wa utawala haramu wa Israel ndio sauti ya madhalimu.
Aidha ameungeza kumusema kumwambia Netanyahu kuwa: umepita njia mbaya kwani Erdogan ni sauti ya wanyonge hali yakuwa wewe ndio sauti ya madhalimu na wakandamizaji.
Naye alibainisha kuwa: kwakuwa mpaka sasa utawala haramu wa Israel haujahukumiwa kutokana na kuendelea kufanya hujuma dhidi ya ubinadamu ambapo ikiwemo kufanya mauaji na kuharibu makazi ya watu, utawala huo hauna haki ya kuzituhumu serikali zingine.
Kwa upande mwengine waziri wa mambo ya nje wa Uturuki pia ametoa ujumbe kufuatia maelezo yaliotolewa na waziri mkuu wa Israel dhidi ya serikali ya Erdogan, nakusema kuwa: Netanyahu ndiye yule ambaye huwauawa watoto ambao hucheza katika fukwe za Gaza na kuuwa idadi kubwa ya Wapelestina wasiokuwa na hatia.   
mwisho/290